Askofu Bagonza aonya dhidi ya ‘sumu’ zinazokwamisha maridhiano

Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Karagwe Dk. Benson Bagonza, amewataka Watanzania kujiepusha na tabia alizozitaja kuwa ni “sumu” tano zinazodhoofisha maridhiano na kuathiri amani ya jamii.

Askofu Bagonza ametoa kauli hiyo wakati wa ibada ya ubarikio wa wachungaji na wadiakonia iliyofanyika katika Dayosisi ya Karagwe mkoani Kagera. Amesema maridhiano ya kweli hayawezi kupatikana iwapo jamii itaendelea kuruhusu mienendo inayochochea migawanyiko.

Akifafanua, amesema sumu ya kwanza ni hila, akieleza kuwa mara nyingi hufichwa chini ya majina ya nia njema au maslahi mapana ya taifa. Amesisitiza kuwa hila huzuia uaminifu na huondoa msingi wa mazungumzo ya kweli.

Sumu ya pili, kwa mujibu wa Askofu Bagonza, ni tabia ya kutafuta ushindi katika mchakato wa maridhiano. Ameonya kuwa maridhiano yanapojengwa kwa mantiki ya mshindi na mshindwa, huacha majeraha yanayoweza kusababisha migogoro na vurugu siku zijazo.

Akiendelea ametaja kukwepa ukweli kuwa ni sumu ya tatu, akisisitiza kuwa maridhiano ya kudumu hujengwa juu ya ukweli ulio wazi, hata pale unapokuwa mgumu au unaoumiza pande husika ambapo amehitimisha kwa kuhimiza jamii kujenga utamaduni wa uaminifu, haki na uwazi ili kuimarisha mshikamano na amani ya kudumu nchini.

#10YrsJembefm  #Familiamoja #AhsantekwaTime

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii