Polisi Babati wachunguza kifo cha mwanaume kijiji cha Mapea

Jeshi la Polisi wilayani Babati mkoani Manyara linafanya uchunguzi kubaini chanzo cha kifo cha Patrick Francis (35), mkazi wa kijiji cha Mapea, aliyefariki dunia nyumbani kwao katika mazingira ambayo bado hayajaeleweka.

Kwa mujibu wa taarifa za awali mwili wa marehemu ulikutwa katika eneo la makazi ya familia alipokuwa akiishi na wazazi wake. Baada ya tukio hilo kugundulika na Jeshi la Polisi lilifika eneo la tukio na kuchukua mwili wa marehemu kwa ajili ya uchunguzi zaidi.

Akizungumza na vyombo vya mwenyekiti wa kijiji cha Mapea alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa mamlaka husika zinaendelea na taratibu za uchunguzi ili kubaini kilichosababisha kifo hicho.

Kwa upande wake, mama mzazi wa marehemu amedai kuwa siku chache kabla ya tukio hilo, mwanawe alionekana kuwa na mwenendo usio wa kawaida na aliwahi kuzungumzia jambo lililompa wasiwasi, hali iliyomfanya kumkanya asijihusishe na vitendo vinavyoweza kuhatarisha maisha yake.

#10YrsJembefm  #Familiamoja #AhsantekwaTime

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii