Unatambua kwamba ulaji wa tufaha (Apple) moja kila siku kunaweza kusaidia kuboresha afya ya moyo kwa kutanua mishipa ya damu, kupunguza uvimbe, kulinda seli, na kusaidia kuweka mishipa ya damu yenye afya, kulingana na utafiti wa karibuni.
Virutubisho Muhimu Vilivyomo Kwenye Tufaha
Tufaha ni tajiri kwa nyuzi za lishe (fiber) na misombo ya mimea inayosaidia kudumisha shinikizo la damu la kawaida na kazi bora ya moyo na mishipa. Zina:
Flavonoids: ikiwemo quercetin na proanthocyanidins
Asidi za phenolic
Nyuzi za lishe
Daktari wa moyo Dr. John Higgins (UTHealth Houston) anasema husaidia moyo kwa njia kadhaa:
1. Kupanua Mishipa ya Damu
Flavonoids huchochea mishipa ya damu kupanuka kidogo, na kufanya damu ipitie kwa urahisi zaidi.
2. Kupunguza Uvimbe
Antioxidants zinazojulikana kama polyphenols hufanya kazi kama viambato vya asili vinavyopunguza uvimbe, kupunguza msongo kwenye mishipa kwa muda, anasema Cassandra Lepore, mtaalamu wa lishe mjini New York.
3. Kulinda Seli
Antioxidants zilizopo kwenye tufaha husaidia kulinda mishipa ya damu dhidi ya uharibifu wa kila siku unaosababishwa na molekuli zisizo imara mwilini.
4. Kusaidia Mishipa ya Damu Iwe na Afya
Nyuzi zinazoyeyuka (soluble fiber) zinaweza kupunguza kiwango cha cholesterol na kudumisha unyumbufu wa mishipa, hivyo kusaidia kudhibiti shinikizo la damu kwa muda mrefu.
5. Kudhibiti Shinikizo la Damu
Hata hivyo Tufaha lina takribani mg 150 ya potasiamu kwa kila tunda linalosaidia unywaji wa potasiamu wa kila siku ambapo Potasiamu husaidia kupumzisha kuta za mishipa ya damu, kupunguza shinikizo la damu, na kulinda misuli dhidi ya kuteseka au kucramp, kulingana na Harvard Medical School.
#10YrsJembefm #Familiamoja #AhsantekwaTime