Rwanda yaishtumu Kongo kwa kuchelewesha mkataba wa amani

Rais wa Rwanda Paul Kagame, ameilaumu serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kwa kuchelewesha kutiwa saini makubaliano ya amani yenye lengo la kumaliza mzozo katika eneo la mashariki lenye utajiri wa madini.

Katika mkutano na waandishi wa habari, Kagame amesema kinachochelewesha makubaliano hayo hakitoki wala hakihusiani na Rwanda.

''Wanakubaliana jambo moja huko Washington au Doha, na hilo linawekwa hadharani. Kisha siku au wiki inayofuata, mtu anasema, hapana hatutafanya hili na hili mpaka hili lifanyike."

Rais huyo ameongeza kusema hana hakika ikiwa watakutana mjini Washington mapema mwezi Desemba na kwamba watasubiri na kuendelea kuwa na matumaini.

Kwa upande wake, ofisi ya rais ya Kongo, imeiambia AFP kwamba mkataba huo wa amani utasainiwa Desemba 4 mjini Washington kati ya Rais wa nchini hiyo Felix Tshisekedi na Kagame ingawa hakuna lolote lililothibitishwa.


#10YrsJembefm  #Familiamoja #AhsantekwaTime

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii