Rais wa Guinea-Bissau aliyepinduliwa madarakani Umaro Sissoco Embalo amekimbilia katika nchi jirani ya Senegal baada ya kuzuiliwa wakati wa mapinduzi ya kijeshi huku mpinzani wake mkuu akimshutumu kwa kupanga uasi.
Taarifa ya wizara ya mambo ya nje ya Senegal, imesema Embalo aliwasili nchini humo kwa ndege ya kijeshi iliyokodishwa na serikali yake.
Hapo jana, katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres alilaani kile alichokiita "ukiukwaji usiokubalika wa kanuni za kidemokrasia" na kutoa wito wa "kurejeshwa mara moja na bila masharti kwa utaratibu wa kikatiba". Haya ni kwa mujibu wa msemaji wake.
Wakati huohuo, Jumuiya ya Kiuchumi ya nchi za Afrika Magharibi ya ECOWAS imesimamisha kwa muda uanachama wa Guinea-Bissau na kutoa wito kwa utawala wa kijeshi kuruhusu tume ya taifa ya uchaguzi kutangaza matokeo ya uchaguzi wa rais uliokuwa na utata.
#10YrsJembefm #Familiamoja #AhsantekwaTime