Baba na Mama Waua Mtato Wao

Jeshi la Polisi mkoani Morogoro linawashikilia watu wawili kwa tuhuma za kumuua na kutupa maiti ya mtoto mchanga katika mto Morogoro, eneo la Mchuma, kata ya Kichangani.

Watuhumiwa hao, Pendo John Matongo (19) na Kumbuka Kwalitaho Barafwa (22), wote wakazi wa Mwembesongo, wanadaiwa kumuua mtoto aitwaye Selina Kumbuka mwenye umri wa wiki tatu.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, SACP Alex Mkama, amesema kuwa uchunguzi wa awali umebaini kuwa mauaji hayo yanatokana na mgogoro wa kifamilia baada ya mwanaume kudai kuwa mtoto huyo si wa kwake.

 Jeshi la Polisi limewashukuru wananchi wema walioripoti kutoweka kwa mtoto huyo na kusaidia kufanikisha kukamatwa kwa watuhumiwa.

#10YrsJembefm  #Familiamoja #AhsantekwaTime

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii