Darasa la Nne kuanza Mitihani ya upimaji kesho

Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) limetangaza kuwa jumla ya wanafunzi 1,582,140 wa Darasa la Nne kutoka shule 20,517 nchini wanatarakiwa kufanya Mtihani wa upimaji wa Taifa wa Darasa la Nne (SFNA) utakaofanyika tarehe   Oktoba 22 na 23 mwaka huu. 

Akizungumza mapema leo Oktoba 21 mwaka huu  jijini Dar es Salaam, Katibu Mtendaji wa NECTA, Prof. Said Ally Mohamed, amesema kati ya watahiniwa hao, wavulana ni 764,290 (asilimia 48.31) na wasichana ni 817,850 (asilimia 51.69).

Ameeleza kuwa asilimia 93.27 ya wanafunzi watafanya mtihani kwa Kiswahili, huku asilimia 6.73 wakitumia Kiingereza, kutegemeana na lugha ya kufundishia inayotumika katika shule zao.

Aidha, jumla ya wanafunzi 5,750 wenye mahitaji maalum wamesajiliwa, wakiwemo wenye uoni hafifu, wasioona, wenye ulemavu wa kusikia, ulemavu wa akili, na ulemavu wa viungo.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii