Watumishi wapatiwa mafunzo juu ya mabadiliko ya mtazamo kwenye eneo la kazi

Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais – UTUMISHI, Bw. Xavier Daudi amesema Serikali inaendelea kuweka mkazo katika kujenga utamaduni wa kazi unaozingatia maadili, ubunifu, na mabadiliko ya fikra miongoni mwa watumishi wa umma.

“Mabadiliko ya kweli katika utumishi wa umma yanaanza kwenye fikra na mitazamo ya mtumishi mmoja mmoja. Tunapaswa kubadilika ili tuwe chachu ya mageuzi katika utoaji wa huduma kwa wananchi,” alisema Bw. Daudi.

Ambapo Oktoba 20 mwaka huu Watumishi wa Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora wamepatiwa mafunzo maalum yanayolenga kubadilisha mitazamo na mienendo yao katika mazingira ya kazi ili kuongeza ufanisi na ubora wa huduma kwa umma.

Mafunzo hayo ambayo hutolewa kila jumatatu yalihusisha mada mbalimbali zikiwemo mbinu za kujitambua, umuhimu wa kuwa na mtazamo chanya, ushirikiano kazini, na namna ya kujenga nidhamu na uwajibikaji katika kutekeleza majukumu ya kila siku ikiwa kwa lengo la kuwajengea uwezo watumishi hao ili kuboresha Utendaji kazi.

Aidha Bw. Daudi amewasisitiza watumishi wa umma kushiriki kikamilifu kwa wale wote ambao waliojiandikisha kwenye daftari la kudumu la mpiga kura kwa ajili ya zoezi la Uchaguzi Mkuu Oktoba 29 mwaka huu kwaajili ya kuchagua viongozi sahihi kuanzia ngazi ya Rais, Ubunge na Udiwani. 

Kwa upande mwezeshaji Mosses Raymond wakati akiwasilisha mada mbalimbali amesema mafunzo hayo yanalenga kuwasaidia watumishi wa umma kuelewa umuhimu wa kujiwekea malengo binafsi na kushirikiana kwa karibu zaidi na wenzao ili kuboresha utendaji wa taasisi.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii