Afisa Mnadhimu Mkoa wa Polisi Tarime Rorya Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Joswam Kaijanante amewataka maafisa usafirishaji maarufu kama Bodaboda wa wilayani Tarime kudumisha na kuilinda amani ya nchi hii.
Ametoa wito huo Oktoba 17 mwaka huu katika kikao cha Jeshi la Polisi Tarime Rorya na Maafisa usafirishaji kilichofanyika katika ukumbi wa TTC Tarime.
Naye Mkuu wa Polisi Jamii Mkoa wa Polisi Tarime Rorya Kamishna Msaidizi wa Polisi Jumanne Mkwama amewataka Bodaboda hao kuendelea kushirikiana na Jeshi la Polisi katika kuimarisha ulinzi na usalama kupitia falsafa ya ulinzi shirikishi.
Aidha Mkuu wa kikosi cha Usalama Barabarani Mrakibu wa Polisi Khamis Wembo aliweza kuwafundisha Bodaboda elimu ya usalama barabarani
Mwishoni Mkuu wa operesheni Mkoa wa Polisi Tarime Rorya Kamishna Msaidizi wa Polisi Festo Ukulule amewataka maafisa usafirishaji kuwa mabalozi katika jamii na kuungana na Jeshi la Polisi katika kukemea wale wote wanaotaka kuvuruga amani yetu tunayojivunia Watanzania.