Idara ya Uhamiaji Wilaya ya Ikungi Mkoani Singida Oktoba 20 mwaka huu imetoa elimu ya Ki-Uhamiaji kwa Jeshi La Akiba (Mgambo) iliyo fanyika katika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya Ikungi.
Elimu iliyotolewa ni pamoja na
1. Majukumu ya Idara ya Uhamiaji.
2. Uraia na aina za Uraia wa Tanzania.
3. Pasipoti, aina za Pasipoti na Hati mbalimbali za kusafiria.
4. Uhamiaji haramu na madhara ya kuwaifadhi wahamiaji haramu.
5. Umuhimu wa kumjua jirani yako.
Elimu hii imetolewa na Kaimu Afisa uhamiaji Wilaya ya Ikungi Mrakibu Msaidizi Vedastus Maingu Masatu, Konstebo Modesta Mayala John pamoja na Konstebo Abdi Mohamed Abdi.
Washiriki walionyesha kufurahishwa na Elimu hiyo na walipata nafasi ya kuuliza maswali na walijibiwa kwa ufasaha .