Wahamiaji haramu wakamatwa Morogoro

Ofisi ya Uhamiaji Mkoa wa Morogoro mwishoni mwa wiki jana imefanikiwa kuwakamata wahamiaji haramu kumi na moja (11) waliyokuwa wamejificha katika msitu uliyopo Kitongoji cha Lachi, Kijiji cha Wami Sokoine, Kata ya Dakawa, Wilaya ya Mvomero Mkoani Morogoro.

Wahamiaji haramu hao walikamatwa kufuatia taarifa za uwepo wao kutoka kwa raia wema ambapo baada ya kuwaona wamejificha msituni walitoa taarifa katika Ofisi ya Uhamiaji Wilaya ya Mvomero iliyowezesha kuwakamata wahamiaji haramu kumi na moja 11 ambapo wahamiaji haramu sita (06) raia wa Bangladesh, raia wa Ethiopia (02), raia wa Somalia (02) na raia wa Burundi (01).

Kukamatwa kwa wahamiaji haramu hao kumethibitishwa na Afisa Uhamiaji Mkoa wa Morogoro Kamishna Msaidizi wa Uhamiaji ACI Saada Natepe, ambae ameendelea kutoa wito kwa Wananchi wa Mkoa wa Morogoro kuendelea kushirikiana na Idara ya Uhamiaji katika utoaji wa taarifa za uwepo wa raia wa kigeni ambao watawatilia shaka.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii