Mazishi ya kitaifa ya Raila Odinga kufanyika Jumapili

Kamati ya kitaifa ya mazishi ya kitaifa ya Raila Odinga, ikiongozwa na Makamu wa Rais Kithure Kindiki, imebainisha kwamba Waziri Mkuu huyo wa zamani atazikwa Jumapili, Oktoba 19, kulingana na matakwa ya familia yake.

Wakati wa kikao na wanahabari mjini Karen kufuatia tangazo la kifo chake siku ya Jumatano, Kindiki amebainisha kuwa Raila alifahamisha familia yake kwamba angependa kuzikwa ndani ya saa 72 baada ya kifo chake.

Makamu wa Rais amebainisha kwamba, kwa mujibu wa tangazo la Rais William Ruto, Raila ataandaliwa mazishi ya kitaifa kwa heshima kamili afisa wa serikali.

"Tunatarajia hatua ya haraka katika siku zijazo kwa sababu iliyowasilishwa na familia baada ya kushauriana na wakili." “Familia ilitufahamisha kuwa Raila alitaka azikwe haraka iwezekanavyo, na wakabaini kuwa muda wa kuzikwa kwake baada ya kifo ni saa 72,” Kindiki amesema.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii