Rais wa zamani wa Honduras Juan akamatwa na polisi

Rais wa zamani wa Honduras Juan Orlando Hernandez amekamatwa na polisi nyumbani kwake kufuatia ombi la Marekani la kutaka kiongozi huyo apelekwa nchini humo kwa makosa yanayohusiana na biashara ya dawa za kulevya na silaha. Kukamatwa kwake kumekuja chini ya wiki tatu baada ya Hernandez kuachia madaraka na madai ya miaka kadhaa ya waendesha mashitaka wa Marekani yanayomhusisha walanguzi wa dawa za kulevya. Siku ya Jumanne, jaji wa mahakama ya juu ya haki nchini Honduras aliyeteuliwa kushughulikia kesi yake, alisaini kibali cha kukamatwa kwa rais huyo wa zamani. Hernandez anatuhumiwa kula njama na makundi ya kusafirisha dawa za kulevya na ufisadi katika taasisi nyingi za umma, kuzorota kwa shughuli za kijamii na kudhoofisha matumizi ya haki nchini Honduras.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii