Kufuatia taarifa zilizoeleza kuwa Odinga ambaye alikuwa amewasili katika eneo la Koothattukulam mkoa wa Ernakulam jimbo la Kerala kwa ajili ya matibabu ya tiba asili ya Kiauyurvedi alianguka ghafla wakati wa matembezi ya asubuhi ndani ya eneo la kituo hicho na kukimbizwa katika hospitali binafsi ya Koothattukulam ambako alithibitishwa kufariki dunia saa 3:52 asubuhi kwa saa za India kwa mujibu wa msemaji wa hospitali ya macho ya Ayurvedic.
Hivyo Waziri huyo wa zamani wa Kenya Raila Amolo Odinga amefariki dunia Jumatano nchini India kutokana na uchunguzi wa madaktari Odinga alikuwa na mshtuko wa moyo kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na polisi na uongozi wa hospitali.
Polisi wamesema mwili wa Odinga umehifadhiwa hospitalini hapo huku taratibu za kidiplomasia zikifanyika kupitia ofisi ya Foreigners Regional Registration Office (FRRO) kwa mujibu wa kanuni za kimataifa.
Msemaji wa hospitali hiyo alibainisha kuwa Raila na familia yake wamekuwa wakiitembelea taasisi hiyo mara kwa mara baada ya kituo hicho kusaidia binti yake kurejesha uwezo wa kuona katika matibabu yaliyopita.