Waziri Mkuu wa zamani wa Kenya Raila Amolo Odinga amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 80 Jumatano wakati akipokea matibabu katika hospitali moja nchini India kwa mujibu wa taarifa zilizothibitishwa na vyombo vya habari vya ndani.
Kifo chake kinakuja kufuatia tetesi zilizokuwa zikisambaa kuhusu hali yake ya afya huku familia yake awali ikikanusha taarifa hizo na kusisitiza kuwa alikuwa katika hali nzuri na anaendelea kupata nafuu ambapo Kaka yake mkubwa ambaye pia ni Seneta wa Siaya Dk. Oburu Odinga aliwatoa hofu Wakenya akisema Raila alikuwa mzima na anapumzika nchini India baada ya kuugua kwa muda mfupi.
Akizungumza na wanahabari Dk. Oburu alikanusha madai kwamba hali ya Raila ilikuwa mbaya huku akizitaja taarifa hizo kuwa zimezidishwa na si sahihi. “Nataka kuwaambia kuwa Raila anaendelea vizuri Kama binadamu mwingine yeyote alikuwa amezidiwa kidogo lakini sasa anapumzika huku akiongeza kuwa hali yake haikuwa mbaya kama ilivyoripotiwa na baadhi ya vyombo vya habari.
Makamu wa Rais Kithure Kindiki na mfanyabiashara mashuhuri SK Macharia ambao ni marafiki wa muda mrefu wa Raila pia waliwatoa hofu wananchi kwa kueleza kuwa walizungumza naye akiwa hospitalini na kueleza kuwa Waziri Mkuu yuko salama na mwenye afya njema.
"Nimezungumza naye mwenyewe na wale wanaomtakia mabaya si watu wema alisema Kindiki pia Macharia naye aliongeza kuwa Asubuhi ya leo nimezungumza naye na jana pia nilimpigia simu hivyo Raila yuko na afya njema na katika siku chache zijazo atarejea nyumbani.”