Umoja wa Ulaya wafikiria wauzaji wengine wa gesi asilia

Rais wa Halmashauri ya Umoja wa Ulaya Ursula von der Leyen amethibitisha kuwa jumuiya hiyo imechukua tahadhari kubwa endapo Urusi itasitisha usambazaji wa gesi katika ukanda huo. Kwa miezi kadhaa jumuiya hiyo imekuwa katika mazungumzo na wauzaji wakubwa wa gesi asilia ikiwa ni pamoja na Marekani, Qatar na Misri ili kuongeza ugavi wake. Majadiliano kama hayo pia yalifanyika na wauzaji wengine kama vile Japan na Korea Kusini. Umoja wa Ulaya umekuwa ukitegemea kwa kiasi kikuwa gesi kutoka Urusi. Tangu Urusi ilipoitwaa rasi ya Crimea mwaka 2014, Umoja wa Ulaya ulipanua mtandao wake wa bomba na kuongeza uwezo wa vituo vya gesi asilia. Kumekuwa na wasiwasi kuwa Urusi inaweza kusitisha usambazaji huo katika hatua ya kulipiza kisasi juu ya vikwazo ilivyowekewa na nchi za magharibi.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii