Ethiopia imeishtumu Eritrea kwa kuungana na vikosi vya Tigray People's Liberation Front (TPLF), kujiandaa kwa ajili ya vita.
Wizara ya Mambo ya nje ya Ethiopia, kupitia barua ilionekana na Shirika la Habari la Ufaransa AFP, inaishtumu serikali ya Eritrea kwa kuimarisha ushirikiano wake na wapiganaji hao.
Aidha, barua hiyo imedai kuwa, Eritrea na TPLF zinapanga vita dhidi ya Ethiopia, kwa mujibu wa barua hiyo iliotumwa kwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres.
TPLF, ambayo kwa miaka 30 ilikuwa inatawala siasa za Ethiopia, imepigwa marufuku kushiriki kwenye shughuli zote za kisiasa, huku uhusiano wa kidiplomasia kati ya Addis Ababa na Asmara ukiendelea kuyumba kwa miezi kadhaa sasa.