Polisi mkoani Njombe wamemkamata Ndugu
Daniel Mwilango Mtuhumiwa wa mauaji ya Nickson Myamba (48) aliyekuwa
katibu wa baraza la walei kanisa la Roman Katoliki kigango cha Parokia
ya Makambako yaliyotokea tarehe 8 February 2022.Mwilango amekamatwa eneo
la Doma wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro.
Kamanda wa polisi
mkoa wa Njombe Hamis Issa amesema mtuhumiwa huyo amekamatwa akiwa na
vitu mbali mbali vya marehemeu ikiwemo simu ya mkononi.
“Katika
hali isiyo ya kawaida simu tuliyomkuta nayo mtuhumiwa ni simu ya
marehemu alikuwa bado anayo yeye,kitu kingine alichokutwa nacho marehemu
ni funguo mbali mbali ikiwemo na ile chumba ambacho tukio
lilitokea”alisema Kamanda Issa
Kamanda Issa amesema mtuhumiwa
huyo amekiri na kuonyesha vitu mbali alivyotumia katika mauaji hayo
ikiwemo Panga aliliokuwa amelitupa katika choo,chuma alichotumia kupiga
marehemu,ndoo na vitambaa vilivyotumika kwa ajili ya usafi wa damu
kwenye chumba yalipotendekea mauaji.
Awali akifafanua juu ya
tukio hilo la mauaji lililotokea katika duka la vitabu lililopo nje
katika eneo la kanisa hilo,kamanda Issa amesema mtuhumiwa alijiandaa na
kutumia chuma kizito kumpiga mwenzake eneo la kisogoni.
“Alipopoteza
fahamu alimuongezea tena chuma kingine pigo la pili na hili pigo la
pili lilimsababishia huyu Nickson Kufariki,alichokifanya huyu Daniel
alitumia panga kuutenganisha mwili,alitenganisha kiwili wili,kichwa na
kifua kilikuwa sehemu yake halafu na kiuno na miguu kilikuwa sehemu
yake”alisema Issa
Vile vile amebainisha kuwa polisi wanamshikilia
mlinzi wa kanisa hilo aliyetambulika kwa jina la Nickson Valentine
kutokana na muunganiko wa kushiriki katika tukio hilo.
“Bado
upelelezi unaendelea lakini sasa hivi mtuhumiwa aliyefanya tukio eneo la
kigango cha kanisa Roman Katoliki eneo la Makambako yuko
Mbaloni”alisema Kamanda
Aidha kamanda Issa amesema jeshi la polisi limebaini kuwa sababu za maujai hayo ni chuki za mtuhumiwa dhidi ya marehemu.
“Hizi
ni chuki binafsi ambazo alikuwa nazo mtuhimiwa dhidi ya marehemu na
ukimuuliza mtuhimwa anasema marehemu ni tishio la maisha yangu kwasababu
amepewa kazi zangu na anamuhisi marehemu ndiye aliyesababisha yeye
akaondolewa kwenye sehemu ya duka na miradi mingine na yeye aliondolewa
kwasababu ya ubadhilifu na sio vinginevyo”alisema Kamanda
Kamanda Issa amesema jeshi la polisi litaendelea kulinda makanisa na kuwaomba waumini kuendelea kwenda kanisani kusali.