Trump amezungumza na Zelensky pamoja na viongozi wa Ulaya

Rais wa Marekani Donald Trump alikuwa na mazungumzo ya njia ya simu mapema Jumamosi na mwenzake wa Ukraine Volodymyr Zelensky pamoja na viongozi wa nchi za Ulaya kuwapa taarifa ya mazungumzo kati yake na Vladimir Putin.

Inaelezwa kwamba Trump alikuwa na mazungumzo ya zaidi ya saa moja kwa njia ya simu na  Zelensky, Waziri Mkuu wa Uingereza Keir Starmer, Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron, Kanasela wa Ujerumani Friedrich Merz, katibu Mkuu wa NATO Mark Rutte na Rais wa kamishene ya Umoja wa Ulaya  Ursula von der Leyen.

Kulingana na taarifa kutoka kwa Ofisi ya Rais wa Ukraine, Trump alizungumza kwanza na Zelensky kabla ya kuwaunganisha viongozi wengine wa bara Ulaya kwenye mazungumzo hayo ya simu.

Mazungumzo kati ya Trump na Putin usiku wa kuamkia Jumamosi katika eneo la Alaska nchini Marekani yalitamatika bila ya kupatikana kwa suluhu ya mzozo wa Ukraine.

Licha ya mazungumzo kati ya viongozi hao wawili kutamatika bila ya mwafaka, walitoa kauli zenye matumaini kuelekea kupatikana kwa amani nchini Ukraine.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii