Kundi la wanamgambo la Hamas limetoa taarifa kuwa, linashauriana na makundi mengine ya Wapalestina kuhusu mapendekezo mapya ya wasuluhishi yanayolenga kusimamisha mapigano katika Ukanda wa Gaza.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo iliyotolewa julai 04, mwaka huu hatua hiyo ni sehemu ya dhamira ya kundi hilo ili kuumaliza uchokozi wa Israeldhidi ya watu wake na kuhakikisha misaada ya kiutu inaingia Ukanda wa Gaza. Limeongeza kuwa litatoa uamuzi wa mwisho kwa wasuluhishi baada ya mashauriano hayo na makundi mengine.
Hamas imetoa kauli hiyo wakati Rais wa Marekani Donald Trump akisema kuwa anatarajia uamuzi wa Hamas kuhusu pendekezo la mwisho la kusitisha vita litatolewa ndani ya saa 24.