Kampeni ya kitaifa ya chanjo na utambuzi wa mifugo yawafikia wafugaji wilayani Longido

Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Mifugo na Uvuvi imeanza utekelezaji wa kampeni ya kitaifa ya chanjo na utambuzi wa mifugo wilayani Longido ambapo takribani mifugo 2000 imechanjwa.

Tukio hilo lililoongozwa na Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Dk Ashatu Kijaji Julai 3, 2025 ikiwa takribani wiki mbili baada ya uzinduzi wa kampeni hiyo uliofanywa na Rais Samia Suluhu Hassan Wilaya ya Bariadi mkoani Simiyu.

Akizungumza wakati wa utekelezaji wa kampeni hiyo, Kijaji amewataka wafugaji wote nchini kutumia fursa hiyo iliyotolewa na Rais Samia kupitia ruzuku ya nusu bei kwa upande wa ng’ombe, mbuzi na kondoo na chanjo bila gharama yoyote kwa upande wa kuku wa kienyeji.

Aidha amewaomba wataalamu wote wa mifugo tusikae ofisini twendeni uwandani tukatatue changamoto zote za wafugaji.


Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii