Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) katika kinachoonekana kupiga hatua katika masuala ya sayansi na teknolojia wamebuni roketi yenye uwezo wa kusafiri umbali mrefu angani na kupeleka vitu mbalimbali.
kwenye maonesho ya Sabasaba yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam mhadhiri wa chuo hicho, Dkt. Phiano Tumaini, amesema roketi ni mafanikio ya masomo ya sayanasi yanayotolewa na chuo hicho.
Amesema roketi ni kama roketi nyingine unazozifahamu ambapo kazi yake kubwa ni kutuma vitu angani pamoja kubeba vitu kama makombora, satellite na vinginevyo na kuendelea kusema;
“Ubunifu ulituchukua miaka kadhaa kuiboresha kwa maana awali ilikuwa unaweza kuituma angani lakini ilikuwa haindi umbali mrefu na wakati mweingine ilikuwa ikipoteza mwelekeo iwapo angani lakini kwa sasa haina changamoto tena”.
Tunawakaribisha wadau mbalimbali waje kwenye banda letu lililopo Viwanja vya Sabasaba ili wajionee mambo mambo mbalimbali ikiwemo mafanikio makubwa ya kisayansi na teknolojia.