Israel waja na mpango mpya kuipindua serikali ya Iran

Israel inaamini kuwa kuna tishio kubwa kutoka kwa nguvu za nyuklia za Iran. Inasema lengo kuu la mashambulizi iliyofanya Ijumaa ilikuwa ni kuharibu tishio hilo.

Ikiwa Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu ana lengo kubwa zaidi kusababisha mabadiliko ya serikali nchini Iran.

Netanyahu anaweza kuamini kwamba kwa kufanya mashambulizi makubwa kuliko hapo awali, anaweza kusababisha mlolongo wa athari zitakazopelekea ghasia, ambazo hatimaye zitasababisha kuanguka kwa Jamhuri ya Kiislamu.

Katika taarifa iliyotolewa ijuma ilieleza kuwa ni wakati wa Wairani kuungana chini ya bendera yao na urithi wake wa kihistoria kwa kusimama kwa ajili ya ukombozi kutoka kwa utawala mbaya na wa ukandamizaji.

Hata hivyo wairani wengi wamechukizwa na hali ya kiuchumi ya nchi hiyo, ukosefu wa uhuru wa kujieleza, na ukiukaji wa haki za wanawake na wachache. Mashambulizi ya Israel yanaonekana kuwa tishio kubwa kwa uongozi wa Iran.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii