Waziri wa sheria nchini Congo atuhumiwa kwa ubadhilifu wa fedha za umma

Bunge la taifa nchini DRC limeidhinisha Mwanasheria Mkuu wa Mahakama ya Juu Juni 15, kumfungulia mashitaka Constant Mutamba ambaya alikuwa Waziri wa Sheria wa DRC  kwa tuhuma za ubadhirifu wa fedha za umma kuhusiana na mradi wa ujenzi wa gereza huko Kisangani, kaskazini mashariki mwa nchi hiyo.

  hivyo waziri huyo anapaswa kujiuzulu wadhifa wake kwa mujibu wa sheria huku akihudhuria hukumu ya watu wanaoshutumiwa kuwa wa kundi lenye silaha la M23 katika gereza la Ndolo huko Kinshasa mnamo Agosti 8, Nchini DRC, wabunge wamefanya uamuzi wao katika kikao cha faraghaa ambapo Kati ya wabunge 363 waliopo, 329 wamepiga kura ya kuunga mkono kumshtaki huyo Constant Mutamba

Constant Mutamba  anatuhumiwa kuhamisha dola milioni 19 kwenye kampuni ya kibinafsi kama sehemu ya kandarasi ya kibinafsi ya ujenzi wa gereza huko Kisangani Mkataba huo ulikuwa wa thamani ya dola milioni 29, 65% ambazo zilikuwa zimelipwa tu, ingawa sheria ya manunuzi ya umma inaweka kikomo cha malipo ya awali hadi 30%. Mkataba huo haukuwa umeidhinishwa na Waziri Mkuu.

Wabunge na mwendesha mashtaka wanaamini kwamba kiasi hiki kingeweza kufujwa ikiwa kitengo cha taifa cha kijasusi cha kifedha hakingezuia akaunti ya walengwa kwa wakati na kutoa tahadhari.

Kampuni inayozungumziwa inaelezewa haijawahi kuwepo na haina ofisi inayojulikana, haina wafanyakazi. Ripoti iliyoidhinishwa na wabunge hao pia inaeleza kuwa eneo ambalo kazi hiyo ingefanywa haipo.

Hata hivyo Bunge pia lilikataa kuchunguza shtaka la pili la mwendesha mashtaka dhidi ya waziri huyo, linalohusiana na mashtaka ya kudharau mahakama na "uchochezi wa kuvunja mamlaka ya umma.


Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii