Katika tukio la kipekee linalodhihirisha mapenzi ya wananchi kwa viongozi wao wakazi wa Mkoa wa Simiyu wamejitokeza kwa wingi kuonyesha furaha na bashasha kuelekea ziara ya Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan inayotarajiwa kuanza tarehe 15 Juni, 2025.
Wananchi hao wameonyesha utayari wa kumlaki Rais kwa shangwe, huku wakieleza kufurahishwa kwao na hatua mbalimbali za maendeleo zinazoendelea kutekelezwa chini ya uongozi wa Serikali ya Awamu ya Sita.
Ziara hiyo ya kikazi ya Mheshimiwa Rais Samia inatarajiwa kuhusisha uzinduzi wa miradi mbalimbali ya kimkakati pamoja na kuzungumza na wananchi, ikiwa ni sehemu ya juhudi zake za kuimarisha huduma za kijamii na kuinua uchumi wa maeneo ya pembezoni kama Simiyu.