Erasto Raphaely Kabupa (50), mkazi wa kijiji cha Igelehedza kata ya Ilembula wilaya ya Wanging’ombe mkoani Njombe amefariki dunia akiwa katika nyumba ya kulala wageni wakati wa kushiriki tendo la ndoa na mke wa mtu.
Tukio hilo limethibitishwa na Kamanda wa Polisi mkoa wa Njombe Mahamoud Banga wakati akitoa taarifa hiyo usiku wa Juni 8 2025, majira ya saa mbili.
Kwa mujibu wa Kamanda Banga marehemu Kabupa aliingia katika nyumba ya kulala wageni inayojulikana kwa jina la Mwendavanu akiwa na mwanamke ambaye jina lake (limehifadhiwa )kwa lengo la kushiriki tendo la ndoa.
Aidha katika harakati hizo marehemu alizidiwa ghafla Baada ya kuzidiwa alikimbizwa katika Kituo cha Afya Ilembula na alifikishwa akiwa tayari amefariki dunia hivyo aliongeza kuwa awali waliingia kwenye gesti kwa lengo la kushiriki tendo la ndoa na hatuna taarifa yeyote ambayo inabainisha wenda kama alitumia dawa.
Kamanda Banga alifafanua kuwa kutokana na aina ya tukio hilo Jeshi la Polisi haliwezi kumkamata mwanamke aliyekuwa na marehemu kwa kuwa visa kama hivyo vimewahi kuripotiwa kwa wanaume walio kwenye ndoa na siyo suala linalohusisha kosa la jinai moja kwa moja.