Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeahirisha kesi ya jinai inayomkabili Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema Tundu Lissu hadi Juni 16, 2025 na kuagiza aendelee kushikiliwa rumande.
Uamuzi huo umetolewa leo na mahakama hiyo baada ya shauri hilo kutajwa mahakamani hapo ambapo upande wa Jamhuri ulimeiomba mahama kuongezewa muda zaidi kwaajili ya kufanya upelelezi huo kukamilika.
Tundu Antiphas Lissu ambaye anakabiliwa na mashtaka mbalimbali huku kesi hiyo inaonyesha dhahiri kufuatiliwa kwa karibu na umma kupitia matangazo ya moja kwa moja kutoka katika vyombo vya kurushia matangazo hivyo kutokana na sababu hizo kesi hiyo itasikilizwa tena juni 16 mwaka huu.
Ili kupata taarifa zaidi endelea kutufuatilia kupitia website yetu ya www.jembenijembe.com kupitia Instagram ,Facebook, tikok,x zamani twitter pamoja na YouTube