Jeshi la polisi limewashikiria waumini wa Kanisa la Ufufuo na Uzima

Kamanda wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam Jumanne Muliro amesema wanawashikilia baadhi ya waumini wa Kanisa la Ufufuo na Uzima la Askofu Josephat Gwajima lililopo Ubungo jijini Dar es Salaam.

Kamanda Muliro amesema hayo leo Jumanne Juni 3, 2025 wakati akizungumza na vyombo vya habari kuhusu kuwakamata waumini hao waliokaidi kanisa hilo kufungwa.

Amesema wao wapo kwa ajili ya kusimamia sheria ambayo imeelekezwa kisheria kinatekelezeka kwa kutokuendelea kufanya shughuli zilizokuwa zikifanyika.

Aidha amesema kama muhusika anataka kuendelea kufanya shughuli ya awali wanatakiwa kufuata utaratibu wa kisheria ikiwa ni pamoja na kukata rufaa kwenye mamlaka za kisheria.

Hatua hiyo imekuja mara baada ya Jana Jumatatu Juni 2, 2025 Serikali kutangaza kulifuta kanisa hilo linalomilikiwa na Askofu Gwajima kwa madai limekiuka Sheria ya Jumuiya Sura ya 337 kwa kutoa mahubiri yenye mwelekeo wa kisiasa na nia ya kuichonganisha Serikali na wananchi.

Ili kupata taarifa zaidi endelea kutufuatilia kupitia website yetu ya www.jembenijembe.com kupitia Instagram ,Facebook, tikok,x zamani twitter pamoja na YouTube 



Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii