Wanasiasa wa Chadema Emmanuela Ntobi ns Glory Tausi waibukia ACT Wazalendo

Wanasiasa wawili waliokuwa sehemu ya kundi la G55 kutoka Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Emmanuel Ntobi na Glory Tausi wamejiunga na ACT Wazalendo.

Hatua ya wawili hao kutimkia ACT- Wazalendo inakuja wiki mbili tangu wanamuungano wenzao wa G55 walipotangaza kujiunga na Chama cha Ukombozi wa Umma (Chaumma).

Akizungumza baada ya hatua hiyo leo Jumanne Juni 3, 2025 Glory amesema anafurahishwa na namna chama hicho kinavyolinda kujali na kuthamini usawa wa jinsia.

Kwa upande wake Ntobi amesema kuwa chama hicho kimeweka wazi mpango wa kushiriki uchaguzi mkuu huku akikiona kuwa jukwaa sahihi kwake kwa kile  alichoeleza kwamba muhuni haususiwi.'

Wawili hao wamekabidhiwa kadi na Katiba za chama hicho na Katibu Mkuu wa ACT Wazalendo Ado Shaibu ikiwa awali Ntobi alikuwa Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Shinyanga kabla ya kusimamishwa kwa kile kilichodaiwa kuwa alifanya kosa la utovu wa nidhamu.

Kwa upande wa Glory ndiye alikuwa mwanzilishi wa programu ya Chadema Digital na aligombea nafasi ya Naibu Katibu Mkuu wa Baraza la Wanawake la Chadema (Bawacha) katika uchaguzi wa ndani wa chama hicho.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii