WAZIRI wa Afya Jenista Mhagama amesema kupitia kampeni za Madaktari Bingwa wa Dk Samia kwa awamu ya kwanza na ya pili jumla ya wagonjwa 154,015 kutoka katika Halmashauri 184 nchini waliweza kupata huduma za ubingwa na ubingwa bobezi.
Ametoa kauli hiyo leo bungeni mjini Dodoma alipokuwa akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya fedha ya Wizara ya Afya kwa mwaka 2025/2026 na kusema kuwa katika kampeni hiyo imesaidis kwa kiasi kikubwa afya ya uzazi na ukunga, watoto wachanga, upasuaji magonjwa ya ndani, kinywa na meno pamoja na usingizi na ganzi.
Aidha kupitia kampeni hiyo jumla ya watumishi wa afya wapatao 9,434 walijengewa uwezo katika kutoa huduma za dharura za uzazi mama na mtoto. Huduma hizo katika awamu zote mbili zimegharimu kiasi cha Shilingi Bilioni 3.8 amesema Waziri Mhagama.