Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS)kupitia ofisi ya Meneja wa Mkoa wa Dar es Salaam umetangaza nafasi sita za ajira za mkataba wa miaka miwili kwa ajili ya usimamizi wa ujenzi wa barabara jijini humo.
Nafasi hizo ni kwa Wahandisi waliobobea katika fani mbalimbali zikiwemo Uhandisi wa Barabara, Miundo Mbinu, Vifaa, na Ramani.
Nafasi zilizotangazwa ni: Resident Engineer, Highway Engineer, Material Engineer, Structures Engineer, Topographical Surveyor, na nyingine, zikiwa na masharti ya kuwa na elimu ya Shahada ya Uhandisi na usajili wa kitaaluma (ERB)Waombaji wanapaswa kuwa tayari kufanya kazi kwa muda mrefu mkoani Dar es Salaam.
Maombi yatakayoambatana na wasifu wa mwombaji (CV) barua ya maombi nakala za vyeti na maelezo ya mawasiliano yatumwe kwa barua pepe au posta kabla ya tarehe 11 Juni 2025, saa 10:30 jioni.
Ili kupata taarifa zaidi endelea kutufuatilia kupitia website yetu ya www.jembenijembe.com kupitia Instagram ,Facebook, tikok,x zamani twitter pamoja na YouTube