Israel imeeleza wazi kuwa Hamas lazima ivunje jeshi lake na mamlaka yake ya kisiasa na kurejesha mateka wote 58 waliobaki kabla ya kukubali kumaliza vita Mpango mpya wa Marekani kwa ajili ya Gaza ulioonekana na Reuters uliopendekeza sitisho la mapigano kwa siku 60 na kuachiliwa kwa mateka 28 Waisraeli (hai na waliokufa) katika wiki ya kwanza, pamoja na wafungwa 125 Wapalestina waliokuwa wamehukumiwa kifungo cha maisha na miili ya Wapalestina 180 waliokufa.
Mpango huo unaodhaminiwa na Rais wa Marekani Donald Trump kwa kushirikiana na wapatanishi kutoka Misri na Qatar, pia unajumuisha kuanza kwa usaidizi wa kibinadamu mara tu Hamas itakapoidhinisha makubaliano hayo.
Hamas itatoa mateka 30 wa mwisho mara tu sitisho la mapigano la kudumu litakapowekwa ikiwa Ikulu ya Marekani imethibitisha kuwa Israel imekubali pendekezo hilo ambapo Kwa upande mwingine Hamas imesema inauchunguza mpango huo na itatoa majibu siku ya Ijumaa au Jumamosi.
Hata hivyo tofauti kubwa kati ya pande hizo mbili zimezuia juhudi za awali za kurejesha sitisho la mapigano lililovunjika mwezi Machi ikiwa Hamas ilikataa kuachana na silaha zake na inataka Israel iondoe majeshi yake Gaza na ijitoe rasmi katika vita hivyo.
Ikumbukwe kuwa mashambulizi ya Israel yalianza baada ya shambulio la Hamas kusini mwa Israel tarehe 7 Oktoba 2023, lililosababisha vifo vya watu 1,200 na mateka 251 kuchukuliwa Kulingana na maafisa wa afya Gaza, kampeni ya kijeshi ya Israel imeua zaidi ya Wapalestina 54,000 na kuharibu vibaya ukanda huo.