MTUNZI WA RIWAYA NA TAMTHILIA GWIJI NGUGI WA THIONG’O AFARIKI DUNIA.

Ngugi wa Thiong’o Mwandishi gwiji wa fasihi kutoka Kenya ameripotiwa kufariki dunia  Mei 28, 2025 akiwa na umri wa miaka 87 ambapo taarifa rasmi zinaeleza kuwa Mwandishi huyo mashuhuri amefariki akiwa Marekani ambako amekuwa akiishi na kufundisha kwa miaka mingi.

Ngũgĩ wa Thiong'o ni mwandishi mashuhuri kutoka Kenya ambaye aliyezaliwa mwaka 1938 katika kijiji cha Kamiriithu eneo la Limuru na kujulikana kwanza kwa jina la James Ngugi kabla ya kuamua kutumia jina lake la Kiafrika hivyo ni mmoja wa waandishi mashuhuri barani Afrika na pia mwanaharakati wa lugha na utamaduni wa Kiafrika.

Hapo awali alianza kuandika riwaya zake kwa Kiingereza lakini baadaye aliamua kuandika kwa lugha ya Kikuyu ili kuendeleza utamaduni na lugha za Kiafrika Kazi zake maarufu ni pamoja na Weep Not, Child (1964), The River Between (1965), na Petals of Blood (1977) Mwaka 1977 alikamatwa na kufungwa kwa sababu ya tamthilia aliyoiandika kwa Kikuyu, Ngaahika Ndeenda ("Nitakupenda Milele"), ambayo ilikosoa serikali.

Baada ya kukamatwa mwaka 1977, Ngũgĩ wa Thiong’o alifungwa katika Gereza Kuu la Kamiti bila kufikishwa mahakamani kwa zaidi ya mwaka mmoja akiwa gerezani aliandika riwaya yake ya kwanza kwa lugha ya Kikuyu iitwayo "Caitaani Mũtharaba-Inĩ" yenye maana ya (Shetani Msalabani)kwa kutumia karatasi za chooni.

Baada ya kuachiliwa kutoka gerezani alikumbwa na vitisho vya ukandamizaji kutoka kwa serikali ya Kenya hali iliyo mlazimu kuondoka nchini na kuishi uhamishoni katika nchi ya Uingereza kisha kukwenda Marekani akiwa uhamishoni aliendelea kuandika na kufundisha na pia kuwa mtetezi mkubwa wa lugha za Kiafrika huku akisisitiza umuhimu wa kuandika katika lugha za asili ili kuendeleza uhuru wa kweli wa kiutamaduni na kisiasa.

Ngugi alitambulika kwa kazi zake mashuhuri alizokuwa akizifanya kama The Black Hermit, Weep Not, Child, The River Between na Petals of Blood pamoja na maandiko ya kiitikadi kama Decolonising the Mind vilevile alikuwa mtetezi thabiti wa matumizi ya lugha za Kiafrika katika elimu na fasihi na alihamasisha uhuru wa kiakili kupitia maandiko yake yenye nguvu ya kisiasa na kijamii.

Mbali na kuwa mwandishi Ngugi pia alikuwa Mwalimu na Mwanafikra ambaye alitoa mchango mkubwa katika vyuo vikuu mbalimbali hasa Chuo Kikuu cha California, Irvine.

Ngũgĩ aliendelea kuwa sauti ya haki, uhuru, na utamaduni wa Kiafrika hadi pale umauti ulipomkuta akiwa pia Profesa katika vyuo vikuu mbalimbali duniani hakika pengo lake litazidi kuacha nafsi kama mwanamapindu wa BaralaAfrika.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii