KAMPUNI YA MAGARI YANAYOTUMIA UMEME CHINA BYD YASHITAKIWA .

Waendesha mashitaka nchini Brazil wameifungulia kesi kampuni kubwa ya magari yanayotumia umeme ya China BYD kwa kuwatumikisha wafanyakazi kwenye mazingira ya utumwa na kuwasafirisha binaadamu kwa njia ya magendo.

Ofisi ya mwendesha mashitaka ya jimbo la Bahia imesema kwenye taarifa yake kwamba inaiomba mahakama kuwa toza fidia ya dola milioni 50 za Kimarekani kwa madhara yaliyosababishwa na kampuni hiyo ya Kichina.

Mashitaka hayo yanatokana na uchunguzi uliofanyika mwaka jana na kupelekea kuokolewa kwa wafanyakazi 220 wa Kichina kwenye kiwanda kipya cha kampuni ya BYD katika mji wa Camacari.

Waendesha mashitaka wanasema wafanyakazi hao waliingizwa nchini Brazil kwa nyaraka na vibali vya uongo.

Msemaji wa kampuni hiyo ameyaita madai hayo kuwa ya uongo na yenye lengo la kuidhalilisha China na bidhaa zake.

Ili kupata taarifa zaidi endelea kutufuatilia kupitia website yetu ya www.jembenijembe.com kupitia Instagram ,Facebook, tikok,x zamani twitter pamoja na YouTube 

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii