Serikali imetangaza kulifutia usajili Kanisa la Ufufuo na Uzima linalomilikiwa na Mbunge wa Kawe Askofu Josephat Gwajima ikiwa ni siku moja tangu kiongozi huyo wa kiroho atangaze msimamo wake wa kuendelea kukemea vitendo vya utekaji na watu kupotea.
Sababu ya uamuzi huo wa Msajili wa Jumuiya za Kiraia Emmanuel Kihampa ni kile kilichoelezwa kanisa hilo limekiuka Sheria ya Jumuiya Sura ya 337, kwa kutoa mahubiri yenye mwelekeo wa kisiasa na nia ya kuichonganisha Serikali na wananchi.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Jumatatu Juni 2, 2025 na Kihampa kitendo kilichofanywa na Askofu Gwajima kinaweza kuhatarisha amani na utulivu nchini.
Wiki moja iliyopita Askofu Gwajima alizungumza na waandishi wa habari huku akikemea vitendo vya utekaji jambo lililozua upinzani kutoka miongoni mwa makada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Jana Jumapili Juni 1, 2025 katika Ibada pamoja na maombi mengine Askofu Gwajima alitangaza maombi ya siku saba kuanzia leo Jumatatu katika makanisa ya Ufufuo na Uzima zaidi ya 2,000 ya kuombea haki na amani.
Ili kupata taarifa zaidi endelea kutufuatilia kupitia website yetu ya www.jembenijembe.com kupitia Instagram ,Facebook, tikok,x zamani twitter pamoja na YouTube