Mabaki ya ndege iliyoanguka Nepal yapatikana

Mabaki ya ndege iliyopotea katika milima ya nchi ya Nepal yamepatikana leo yakiwa yamepatapakaa na watu 14 kati ya 22 waliokuwemo kwenye ndege hiyo wakathibitishwa kufariki dunia. Haya yamesemwa na jeshi la nchi hiyo. Hakujatolewa tamko lolote kuhusiana na walionusurika ajali hiyo ingawa shughuli ya kuwatafuta bado inaendelea katika eneo hilo la tukio. Raia wawili walikuwa kutoka Ujerumani na wanne kutoka India, huku wahudumu watatu wa ndege hiyo na abiria wengine wote wakiwa raia wa Nepal. Ndege hiyo ilianguka Jumapili iliyopita katika eneo lenye mito mingi na milima na safari hiyo ilikuwa inatakiwa kudumu kwa dakika ishirini tu.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii