Watu 80 wamekufa kwa mripuko Nigeria

Watu 80 wameteketea kwa moto kufuatia mripuko uliotokea usiku katika kiwanda kinachochakata mafuta kinyume cha sheria Kusini mwa Nigeria. Taarifa hii ni kwa mujibu wa kitengo cha kukabiliana na matukio ya dharura.Mwakilishi wa kitengo cha taifa hilo cha kukabiliana na majanga (NEMA), Ifeanyi Mnaji ameliambia shirika la habari la Ufaransa AFP kwamba miili ya watu hao 80 imekutwa imeteketea kwa moto katika eneo la tukio.Amesema pia katika eneo hilo kumeshuhudiwa kutapakaa kwa magari yalioungua vifaa vya kuchotea mafuta, vilivyotumika kuibia mafuta ghafi na petroli. Vyombo vya habari nchini Nigeria vimesema zaidi ya watu 100 wamekufa kutoka na mripuko huo.Usafishaji haramu wa mafuta ni jambo la kawaida katika ukanda huo wa mafuta ambako wezi huharibu mabomba ili kuiba mafuta ghafi ambayo wanayasafisha ili kuyauza kwenye soko la magendo.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii