Maduka 17 katika eneo la Buseresere wilayani Chato, Mkoa wa Geita yameteketea kwa moto ambao chanzo chake hakijafahamika.
Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji mkoani Geita, Hamis Dawa amethibitisha kutokea kwa moto huo akisema taarifa zaidi atazitoa muda mfupi ujao.
Kwa mujibu wa mashuhuda moto huo ulizuka saa tatu usiku ambapo wamedai ulianza kwenye duka moja linalouza vifaa vya umeme kabla ya kusambaa kwenye maduka mengine na kusababisha uharibifu wa mali.
Baadhi ya wafanyabiashara wa maduka hayo wamelalamikia kuchelewa kwa gari la zimamoto hivyo kuperekea moto huo kusambaa kwa kasi zaidi na kusababisha hasara ambapo Moto huo umefanikiwa kuzimwa na wananchi wakishirikiana na Jeshi la Zimamoto.