Baadhi ya majengo ya Shule ya Sekondari ya Jenista Mhagama iliyopo Halmashauri ya Songea yameungua kwa Moto ikiwemo Mabweni ya Wanafunzi wa kike na Stoo ambapo imelidai kuwa moto huo umetokana na hujuma
Mkuu wa Wilaya Wilman Ndile, alipoulizwa kuhusu tukio hilo amesema Moto umesababisha hasara kubwa na umeharibu majengo, Chakula cha Wanafunzi cha thamani ya Tsh. Milioni 1, vingine vilivyoungua ni Magodoro na Vifaa ya Umeme
Aidha DC amesema kuwa Mwanafunzi huyo alichoma Moto shule mara tatu kwa siku tofauti, Mei 31, Juni 1 na Juni 3, 2025, kwa sasa anashikiliwa na anatarajiwa kupelekwa Mahakamani na wemezungumza na Wazazi wake nao pia wamekiri kuwa Mtoto huyoa ni mkorofi.