Wapalestina 10 wauawa wakati wakitafuta msaada kusini mwa Gaza

Shirika la ulinzi wa raia wa Gaza limesema mashambulizi ya Israel  siku ya jana Jumapili yamewaua takriban watu 10 wakiwemo wasichana wawili katika Ukanda huo.

Msemaji wa shirika hilo Mahmud Bassal amesema miili ya watu waliouawa na majeruhi wamepelekwa katika Hospitali ya Nasser iliyo katika mji wa kusini wa Gaza Rafah.

Watu hao walikuwa wakielekea katika kituo cha usambazaji wa misaada kinachoshukiwa kuwa na uhusiano na Israel na kinachoungwa mkono na Marekani GHF wakati vikosi vya Israel vilipowafyatulia risasi kwa madai kwamba walikatiza katika maeneo yasiyoruhisiwa ya vikosi vyao.

Hayo yanajiri wakati waziri wa ulinzi wa Israel Israel Katz akisema kwamba ameliagiza jeshi kuuzuia msafara wa misaada unaomjumuisha mwanaharakati wa mazingira wa Sweden Greta Thunberg, kutokutia nanga kwenye Ukanda wa Gaza.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii