Waandamanaji wanaopinga sera za Uhamiaji wazidi kuandamana kwa siku tatu

Maandamano yamezidi kupamba moto kwa siku ya tatu huko Los Angeles, ambako waandamanaji wanaopinga sera za uhamiaji za Rais wa Marekani Donald Trump wamekabiliana na maafisa wa usalama.

Wanajeshi wa kikosi maalum waliotumwa na Rais Trump mjini humo licha ya pingamizi kutoka kwa Gavana wa jimbo la California na Meya wa mji wa Los Angeles wametumia gesi ya kutoa machozi na risasi za mpira kukabiliana na waandamanaji hao.

Meya wa Los Angeles Karen Bass amesema machafuko katika jiji hilo yaliyochochewa na utawala huku Gavana wa California Gavin Newsom akisema kuwa uamuzi wa Donald Trump kupeleka Walinzi wa Kitaifa kwenye maandamano hayo ndio uliozidisha ghasia hizo.

Waandamanaji walikusanyika karibu na eneo ambapo maafisa wa Uhamiaji na Utekelezaji wa Forodha walifanya uvamizi siku ya Jumamosi na kufunga barabara kuu .

Democrats walitaja vitendo vya Trump kuwa   matumizi mabaya ya mamlaka ni mara ya kwanza kwa rais wa Marekani kupeleka Walinzi wa Kitaifa katika jimbo bila ombi kutoka kwa gavana wa eneo husika.

Rais wa Marekani Donald Trump ameonya kuwa kutakuwa na wanajeshi kila mahali ikiwa maandamano yataendelea na kuongeza kuwa hawatoacha nchi yeo isambaratike

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii