Mwanaume mmoja aliyefahamika kwa jina la Odilo Anania Sumi (80), fundi ujenzi mkongwe, amekutwa amefariki dunia katika eneo la makaburi ya Kola, Manispaa ya Morogoro, huku mwili wake ukiwa umeharibika.
Tukio hilo limetokea Juni 5, 2025 majira ya asubuhi, huku mashuhuda wakieleza tukio hilo ni la kwanza kutokea katika eneo hilo hali iliyozua taharuki.
Aidha, Marehemu alikutwa na vitu kadhaa ambavyo ni pamoja na simu ya mkononi, dawa na nguo.
Kwa Mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Juni 6,2024 na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro SACP Alex Mkama, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kueleza kuwa uchunguzi wa awali umebaini kuwa marehemu hakuwa na makazi rasmi.
Jeshi la Polisi mkoa wa Morogoro limetoa wito kwa jamii kuwahifadhi na kuwatunza wazee, likisisitiza kuwa vitendo vya kuwatupa na kuwasahau wazee vinaweza kusababisha matukio ya kusikitisha kama haya.