Kutokana na tangazo la Donald Trump kufuta nchini 12 kuingia nchini Marekani ikiwemo nchi ya Chad rais wa Chad Mahamat Idriss Deby maarufu Jenerali Kaka amesema Chad haina mabilioni ya fedha wala ndege za kugawa misaada kwa nchi nyingine ikiwemo Marekani lakini ina heshima, utu na fahari ambavyo nchi hiyo itavilinda kwa nguvu zote.
Mahmat amesema hayo wakati akitoa majibu ya kujibu mapigo kuhusu tangazo la Trump la kuwawekea mipaka Raia wa nchi 12 kuingia nchini Marekani ambapo Mataifa hayo ni Afghanistan, Myanmar, Chad, Kongo, Guinea ya Ikweta, Eritrea, Haiti, Iran, Libya, Somalia, Sudan na Yemen.
Katika hatua hiyo ya kulipiza kisasi Mahamat amepiga marufuku Raia wa Marekani kupewa viza ya kuingia Chad, Mahamat alichukua madaraka April 2021 kufuatia kifo cha Baba yake, Idriss Dérby, aliyefariki baada ya kujeruhiwa katika mapigano kwenye uwanja wa vita.
Itakumbukwa hivi karibuni utawala wa Rais Donald Trump ulikubali zawadi ya ndege aina ya Boeing 747 kutoka Serikalu ya Qatar, na tayari umeagiza jeshi la anga kufanya tathmini juu ya uwezekano wa kuiboresha kwa matumizi ya baadaye kama Air Force One, ndege hiyo hasa ikizingatiwa imetolewa muda mfupi baada ya ziara ya Trump nchini Qatar, ambako alisaini mikataba ya kibiashara.
Trump pia hivi karibuni alipokutana na Rais wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa katika Ikulu ya White House nchini Marekani alimuuliza pia kama Afrika Kusini inaweza kuipa ndege Marekani lakini Ramaphosa alisema Afrika Kusini haina uwezo wa kuipa Marekani ndege.