Urafiki wa Rais wa Marekani Donald Trump na mfanyabiashara tajiri zaidi duniani Elon Musk, sasa unaonekana kumalizika baada ya wawili hao kutupiana cheche za maneno makali kwenye mitandao ya kijamii.
Rais wa Marekani Donald Trump anasema ameshangazwa sana na kukatishwa tamaa na ukosoaji wa mshirika wa zamani Elon Musk, kuhusu Muswada wake mkuu wa bajeti.
Aidha Trump aliwaambia waandishi wa habari katika Ikulu ya White House siku ya jana baada ya kauli yake Musk alijibu kwa ujumbe mkali,alimshutumu rais Trump kwa kutokuwa na shukran na kuongeza kuwa bila yeye Trump angepoteza uchaguzi.
Musk aliacha wadhifa wake katika Wizara ya Ufanisi wa Serikali wiki iliyopita baada ya siku 129 kazini lakini katika siku chache tangu aondoke mamlakani amekuwa akiukosoa mara kwa mara Muswada wa bajeti ya Trump unaofanya kazi kupitia Bunge la Congress akiuita wa kuchukiza na kuchapisha kwenye ukurasa wake wa X.