Trump ametia saini mataifa 12 kutoingia nchini Marekani.

Rais wa Marekani Donald Trump ametia saini tangazo la kupiga marufuku Raia wa Mataifa 12 kuingia nchini humo akitaja sababu kuwa ni kulinda usalama wa Taifa, Vyombo vya habari vva nchini Marekani vimeripoti taarifa hiyo vikiwanukuu Maafisa wa utawala wa Trump.

Tangazo hilo linalowazuia kabisa na kuwawekea mipaka Raia wa nchi hizo kuingia nchini Marekani, ambapi Mataifa hayo ni Afghanistan, Myanmar, Chad, Kongo, Guinea ya Ikweta, Eritrea, Haiti, Iran, Libya, Somalia, Sudan na Yemen.

Huku Raia wa Mataifa mengine saba ya Burundi, Cuba, Laos, Sierra Leone, Togo, Turkmenistan na Venezuela watawekewa zuio la kiwango fulani.

Itakumbukwa wakati wa muhula wake wa kwanza, Trump aliwapiga marufuku wasafiri kutoka mataifa saba yenye idadi kubwa ya Waislamu kuingia Marekani, hatua ambayo hata  ilipata ukinzani wa kisheria na ilionekana kubatilishwa na Rais Joe Biden mnamo mwaka 2021, akisema imelitia doa Taifa hilo

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii