Dkt, Ndumbaro amazitaka sheria zifuatwe kipindi cha kampeni za uchaguzi

WAZIRI wa Katiba na Sheria Dk Damas Ndumbaro amesema kuwa sheria za nchi haziendi likizo wakati wa kampeni za uchaguzi bali zinakuwepo  na kila mwananchi anapaswa kuzitii kama inavyotakiwa.

Dk Ndumbaro ameyasema hayo Juni 03, 2025 wakati akifungua mafunzo ya sita ya mawakili wa serikali zaidi ya 600 kutoka  wizara, taasisi na mamlaka mbalimbali za umma.

Dr ndumbaro amesema Mwaka huu ni mwaka wa uchaguzi kuna mengi yatasikika lakini katika kipindi hiki cha kampeni huwa anajiuliza kuwa  sheria zinakwenda likizo? Kwasababu kunq watu wanajiamisha uvunjifu wa sheria utakaotokea kipindi cha kampeni sio uvunjifu wa sheria kwa sababu tu unafanywa na wanasiasa.

Ameongeza kuwa Kwa uelewa wake wa sheria kipindi cha kampeni sheria haziendi likizo, sheria zipo zinafanya kazi, wanasheria wapo wanafanya kazi na  mahakama zipo zinafanya kazi.

Aidha, Dk Ndumbaro amewataka mawakili  hao kuwaelimisha wanasiasa juu ya kuzingatia sheria katika kipindi cha kampeni kama ambavyo Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ibara 13 (1) inavyo zungumzia usawa mbele ya sheria.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii