Kesi ya rufaa ya Nyundo na wenzake inaendelea leo Mahakamani Dodoma

Mawakili wa serikali na wale wa upande wa utetezi wamejiandaa kwa kusikilizwa kwa kesi ya rufaa inayowakabili Nyundo na wenzake, waliokata rufaa kupinga adhabu ya kifungo cha maisha gerezani waliyopewa Septemba 30, 2024. Watuhumiwa hao walihukumiwa baada ya kupatikana na hatia ya kumbaka kwa kikundi na kumwingilia kinyume na maumbile msichana mkazi wa Yombo Dovya  jijini Dar es Salaam.

Kwa upande wa utetezi mawakili wakiongozwa na Wakili Godfrey Wasonga wamefika mahakamani wakiwa na mabegi matano yenye vitabu mbalimbali vya kisheria ambavyo vitatumika kama rejea katika kujenga hoja za kupinga hukumu hiyo.

Shauri hilo linasikilizwa leo Jumanne Juni 3, 2025 katika Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dodoma mbele ya Jaji Amir Mruma.

Ili kupata taarifa zaidi endelea kutufuatilia kupitia website yetu ya www.jembenijembe.com kupitia Instagram ,Facebook, tikok,x zamani twitter pamoja na YouTube 


Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii