Mkuu wa Dawati la Jinsia na Watoto Dodoma Mratibu Msaidizi wa Polisi ASP Crister Kayombo amewataka waumini wa kanisa la Waadventista Wasabato Msangalalee Jijini Dodoma kusimamia misingi ya malezi kwa watoto na kuepukana na vitendo vya ukiatili dhidi ya watoto hao.
ASP Kayombo ameyasema hayo Mei 17,2025 katika kanisa hilo wakati akizungumza na waumini katika sherehe ya siku ya Chama cha wavumbuzi Duniani ambapo aliongozana na wadau kutoka Shirika la (ADRA) linalotoa misaada kwa watu wenye uhitaji katika jamii ikiwemo walemavu wangozi ambapo ameiasa jamii kumrudia mwenyezi mungu na maandiko ya vitabu vya dini.
Aidha, kwa upande wake Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Zuhura Muhuji kutoka Dawati la Jinsia na Watoto Dodoma amekemea vitendo vya wazazi na walezi kutoa adhabu kali kwa watoto ambazo zimaweza kuwasabishia madhara pamoja ulemavu, jambo ambalo ni kinyume na sheria.
Vilevile shirika la (ADRA) limepongeza jeshi la polisi kwa kuendelea kushirikiana kutoa elimu kwa jamii dhidi ya mapambano ukatili ikiwemo vitendo vya ukatili kwa watu wenye ulemavu huku akisisitiza jamii kushiriki siku ya tarehe 21/06/ 2015 kuchangia watu wenye uhitaji.