Kwa mwaka 2024/2025 Matukio ya vitendo vya ukiatili wa kijinsi na makundi maalum vimepungua

Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia Wanawake na Makundi Maalumu  amesema wizara yake imeshughulikia migogoro ya ndoa 97,234 katika kipindi cha Julai hadi kufikia Aprili 2025 kupitia Kitengo cha Ustawi wa Jamii ngazi ya halmashauri hadi taifa.

Ametoa takwimu hizo leo Jumanne Mei 27, 2025, bungeni jijini Dodoma Dkt Dorothy Gwajima alipokuwa akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya wizara yake kwa mwaka wa fedha 2025/26.

Pia amesema kuwa mashauri 81, 820 yalipatiwa ufumbuzi 15,414  na kupelekwa mahakamani kwa hatua zaidi huku wizara hiyo kwa kushirikiana na wizara za kisekta na wadau imeendelea kuratibu huduma kwa manusura wa vitendo vya ukatili wa kijinsia na ukatili dhidi ya watoto.

Aidha ameeleza kuwa katika kipindi cha Julai 2024 hadi Aprili 2025, manusura 19,717 waliripotiwa wakiwemo watoto 7,278, wa kiume 1,373 na wa kike 5,905 na watu wazima 12,439 ambao wote walipata huduma katika madawati ya jinsia na watoto ya polisi nchini ambapo pia maofisa ustawi wa jamii huwa wapo kwajili ya ufuatiliaji wa kina.

Dk Gwajima amesema vitendo vya ubakaji vimepungua kutoka matukio 8,185 mwaka 2023 hadi 7,670 sawa na kupungua kwa asilimia 6.3, huku matukio ya ulawiti yakipungua kutoka matukio 2,382 mwaka 2023 hadi 1.930 sawa na kupungua kwa asilimia 9 mwaka 2024 .

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii