Manispaa ya Lindi kupokea rasmi Mwenge wa Uhuru leo

Mwenge wa Uhuru umeingia rasmi katika Manispaa ya Lindi leo mei 27.2025 baada ya kupokelewa na Mkurugenzi wa Manispaa hiyo Juma Mnwele katika viwanja vya Shule ya Msingi Mnazi Mmoja Mwenge huo ulikabidhiwa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mtama Anderson Msumba kufuatia kukamilika kwa mbio zake katika halmashauri hiyo.

Akizungumza wakati wa mapokezi Mkurugenzi Mnwele amesema Mwenge wa Uhuru katika Manispaa ya Lindi utakimbizwa katika majimbo mawili ya Mchinga na Lindi Mjini ambapo utakagua na  kuzindua pia  kuweka mawe ya msingi kwenye miradi saba yenye thamani ya Shilingi Bilioni 2.8.

Mbio hizo zitafanyika kwa umbali wa kilomita 228.7 na zinatarajiwa kuhamasisha maendeleo, mshikamano na uzalendo miongoni mwa wananchi wa Manispaa ya Lindi.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii